Mkopo wa Kopa Ada
Jina La Mkopo
Mkopo wa Kopa Ada
Lengo la Mkopo
Kutoa msaada wa kifedha kwa wanafunzi ambao bila hilo wangeshindwa kuhudhuria shule kwa kukosa ada.
Kusaidia wazazi na walezi kulipa ada kwa wakati mara zote.
Kusaidia shule ziwe na ukwasi wa kutosha (sufficient liquidity) kuendesha shughuli zao bila usumbufu.
Walengwa
Wazazi/Walezi wenye watoto katika shule za msingi na za sekondari.
Maelezo/Vipengele vya Mkopo
Muda Wa Mkopo: Kuanzia muhula 1 Mpaka mihula 3
Ratiba ya Mrejesho
Kila mwezi
Kiwango Cha Mkopo:
Kuanzia TZS 100,000 Mpaka TZS 3,000,000 kutegemeana na mpangilio wa ada wa shule husika.
Mahitaji ya Kuwasilisha Kufanya Tathmini ya Mkopo
- Mkataba wa Makubaliano (MOU) na shule husika.
- HifadhiData (Database) ya wazazi/walezi wote kutoka shule.
- Fomu ya Maombi ya Mtandao iliojazwa kikamilifu.