Mkopo wa Mtaji
Lengo la Mkopo
Kusaidia Biashara Ndogo na za Kati (MSME’s) kwa mahitaji ya mtaji wa kila siku wa kazi (Working Capital).
Kusaidia taasisi/kampuni/mfanyabiashara kupata vifaa (assets) mbalimbali wanazohitaji za kusaidia kuboresha na kukuza biashara zao.
Walengwa
Taasisi Ndogo na za Kati za Biashara (MSMES’s) kama vile Makampuni, Kampuni za Ushirikiano (Partnership firms) na za Umiliki wa mtu mmoja (Single Proprietorship firms).
Maelezo/Vipengele vya Mkopo
Muda wa Mkopo: Mpaka miezi 24 .
Ratiba ya Mrejesho
Kila mwezi
Kiwango Cha Mkopo:
Kopa kuanzia TZS Milioni 1 Mpaka TZS Milioni 30.
Mahitaji ya Kuwasilisha Kufanya Tathmini wa Mkopo
Kampuni ya Umiliki Binafsi (Single Proprietorship)
- Leseni hai ya Biashara ya Manispaa/Halmashauri.
- Usajili wa Biashara (Pale Inapostahili).
- Nakala ya Cheti cha Mlipa Kodi (TIN Certificate).
- Hati Safi ya TRA (Tax Clearance Certificate).
- Ushahidi wa Umiliki.
- Taarifa ya Ukaguzi wa Fedha (Pale Inapostahili) au Mahesabu ya Biashara isiopungua mwaka mmoja nyuma.
Kampuni ya Dhima Yenye Kikomo (Limited Liability Company)
- Leseni ya Biashara (Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara).
- Hati ya Usajili Kampuni (BRELA).
- Hati/Memoranda na Makala ya Makubaliano - Memorandum and Articles of Association (MEMART).
- Nakala ya Cheti cha Mlipa Kodi cha Kampuni (Company TIN Certificate).
- Hati Safi ya TRA (Tax Clearance Certificate).
- Azimio la Bodi/Wakurugenzi/Menejiment kukopa.
- Taarifa ya Ukaguzi wa Fedha (Pale Inapostahili) au Mahesabu ya Biashara isiopungua mwaka mmoja nyuma.
Kampuni ya Umiliki wa Pamoja (Partnership Firm)
- Hati ya Ubia (Partnership Deed).
- Hati ya Usajili wa Kampuni (BRELA).
- Hati/Memoranda na Makala ya Makubaliano - Memorandum and Articles of Association (MEMART).
- Nakala ya Cheti cha Mlipa Kodi cha Kampuni (Company TIN Certificate).
- Azimio la Wabia kukopa.
- Hati Safi ya TRA (Tax Clearance Certificate).
- Taarifa ya Ukaguzi wa Fedha (Pale Inapostahili) au Mahesabu ya Biashara isiopungua mwaka mmoja nyuma.