Mkopo wa Pamoja
Lengo la Mkopo
Kukidhi mahitaji ya Wajasiriamali wanaoendesha Biashara Ndogo ndogo (Micro and Small Businesses) ya mtaji wa kazi wa kila siku (Working Capital).
Walengwa.
Mjasiriamali Mmoja-mmoja anaedhaminiwa na wanakikundi wenzake.
Maelezo/Vipengele vya Mkopo
Muda wa Mkopo: Mkopo wa Kwanza miezi 3 -6. Mkopo wa Pili Mpaka miezi 12.
Ratiba ya Mrejesho
Kila wiki au mara mbili kwa wiki.
Kiwango Cha Mkopo
- Mkopo wa kwanza: TZS 100,000 - 500,000
- Mkopo wa Pili: Mpaka TZS 1,000,000
- Mkopo wa Tatu: Mpaka TZS 2,000,000
- Mkopo wa Nne: Mpaka TZS 3,000,000
Mahitaji ya Kuwasilisha Kufanya Tathmini wa Mkopo.
- Mkopaji atimize vigezo vya ustahili.
- Barua ya kumpendekeza mkopaji kutoka kamati ya mikopo ya kikundi.
- Historia ya mikopo iliopita (marejesho na tabia).
- Historia ya mzunguko wa fedha inayokidhi kufanya marejesho ya mkopo.
- Lazima mkopaji apitie mafunzo ya SELF MF kuhusu uzoefu/uelekeo wa mikopo (Loan Orientation Training).
- Afisa mikopo wa SELF MF lazima aridhike kwamba mwombaji wa mkopo anaelewa vema maelezo na masharti ya mkopo.